Work and Wages

Minimum Wage

Kulingana na katiba ya Tanzania, kila mtu, bila ubaguzi wa aina yeyote, ana haki ya kupata ujira kutokana na kazi na wote wanaofanya kazi, wanapaswa kupata stahiki zao za malipo kwa kadiri ya utendaji na sifa za kufanya kazi husika. Kila mtu ana haki ya kupata malipo stahiki.

Viwango hivi huwekwa na Bodi za mishahara za kisekta ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria ya kazi ya mwaka 2007. Ili kufikia viwango vya chini vya mshahara, bodi za mishahara za kisekta huzingatia vigezo muhimu kama vile gharama za maisha; hali ya mishahara nchini; uzalishaji; uwezo wa waajiri kuendesha biashara zao vizuri utekelezaji kazi wa shughuli za kibiashara za kati; ndogo na ndogo sana; biashara mpya; gharama za kuishi; kupunguza umaskini; kiwango cha chini cha kujikimu; malipo na makubaliano na masharti ya ajira kwa waajiriwa wa sekta ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Makubaliano yoyote ya pamoja ya malipo na mapatano na masharti ya ajira kwenye sekta. Tukio la sharti lolote la ajira lililopendekezwa kwa ajira ya wakati huo au uuandaaji wa ajira.

Kwa sasa kuna viwango vya chini vya mshahara kwa sekta zifuatazo: Ujenzi, shule binafsi, nishati, viwanda na biashara, hoteli na huduma za majumbani, Nyingine ni ulinzi binafsi, madini, afya, uvuvi, usafirishaji, mawasiliano na kilimo na nyingine zisizo tajwa hapa. 

Ridhaa ya Kima cha Chini inasimamiwa kupitia Idara ya Usimamizi Kazi na Huduma za Ukaguzi ambayo iko chini ya Wizara ya Kazi na Ajira. Idara inasimamiwa na Kamishna wa Kazi. Maafisa wa Kazi chini ya idara hii wamewezeshwa na Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004 ili kusimamia ridhaa na viwango vya ajira ikiwa ni pamoja na Agizo la Kima cha Chini na sheria na masharti mengine ya ajira.

Kwanza kabisa ikiwa Afisa wa Kazi anaamini ya kwamba mwajiri hajafuata sheria za kazi anaweza kutoa agizo la ridhaa na ikiwa mwajiri anashindwa kufuata agizo la kisheria mwajiri atashtakiwa na akifungwa atalipa faini isiyozidi Shilingi Millioni Tano, kifungo cha kipindi cha miezi 3 au zote faini na kifungo. Hii ni kulingana na kitengo 64 (2) cha Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004.

uhusika uko katika kiwango cha ukaguzi, wakiwa katika maeneo ya kazi Wachunguzi wa Kazi uhoji wafanyakazi au chama cha wafanyakazi ikiwa wako na mwakilishi wa usimamizi. Hata hivyo ikiwa kuna mzozo wa haki au wafanyakazi waliosajiliwa chini ya chama cha wafanyakazi wanaweza kwenda kwa Tume kwa Upatanisho na Usuluhishi kupitia tawi lao. Waajiri pia wanaweza kwenda kwa Tume kwa Upatanisho na Usuluhishi kupitia mashirika ya waajiri wao.

Watu binafsi wanaweza kulalamika au kuripoti mzozo ili kudai baki kwa Tume la Upatanisho na Usuluhishi (CMA) wenyewe au kupitia vyama vyao vya wafanyakazi. CMA ni taasisi ya kazi iliyoanzishwa chini ya sehemu ya 12 ya Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004 na kazi ya kupatanisha mzozo wowote uliotajwa katika masharti ya sheria yeyote ya kazi; kuamua mzozo wowote uliotajwa na Usuluhishi. Kamshina wa Kazi 12 chini ya sehemu 47 (8) ya sheria ya taasisi ya kazi, 2000 inatumika kwa Mahakama ya Kazi kulazimisha ufuataji ikiwa mwajiri hajafuata agizo.  Na ridhaa yake inaweza kuripotiwa katika mahakama ya Kazi pia kulingana na Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004. 

Vyanzo: § Sehemu ya 23 ya Katiba ya Tanzania; § Sehemu ya 37 ya Sheria za Taasisi za Wafanyakazi ya 2004

Kwa kima cha chini kilichosasishwa cha mshahara, rejelea sehemu ya Kima cha Chini cha Mshahara.

Regular Pay

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004 hutofautisha kati ya "ujira" na "mshahara wa kawada". Ujira ni thamani kamili ya malipo yote, kipesa au kwa njia yoyote, inayolipwa mfanyakazi kutokana na ajira ya mfanyakazi huyo. Mshahara wa kawaida humaanisha sehemu ya ujira wa mfanyakazi huo unaolipwa kuhusiana na kazi iliyofanywa wakati wa saa za kawaida za kufanya kazi lakini haijumuishi marupurupu (iwe inategemea mshahara wa kawaida wa mfanyakazi au la) na malipo ya kazi ya ziada.

Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini husimamia malipo ya mishahara kwa wafanyakazi wa aina yoyote. Kulingana na Sheria hii, mishahara inaweza kuhesabiwa kwa saa, kila siku, kila wiki, au kila ,wezi. Wafanyakazi walioajiriwa mara kwamara badala ya muda wa kufanya kazi hulipwa kila wiki na mishahara yao uhesabiwa kwa msingi wa kiwango wastani ulichokipata kwa kipindi cha wiki 13 au kulingana na muda wao wa ajira (ikiwa ni chini ya wiki 13).

Waajiri wanawajibika kumlipa mfanyakazi mshahara wake wa saa alizofanya kazi katika eneo la kazi kulingana na siku ya malipo katika bahasha iliyofunika, ikiwa malipo yatakuwa kwa pesa taslimu au kupitia cheki.  Mshahara unaweza kuweka moja kwa moja kwenye akaunti iliyoteuliwa na mfanyakazi kwa kuandikwa. Waziri anayewajibika kwa masuala ya kazi anaweza kuruhusu malipo nusu ya mshahara kwa matumizi ya kibinafsi kwa mfanyakazi na familia yake.

Kwa ujumla, mwajiri haruhusiwi kupunguza mishahara isipokuwa iki inahitajika au imeruhusiwa chini ya sheria iliyoandikwa, makubaliano ya pamoja, uamuzi wa mshahara, agizo la mahakama au tuzo la maombi ya rufaa. Kipunguzo kinaweza pia kufanywa ikiwa mfanyakazi atakubali kipunguzo hicho kwa kuandika kuhusiana na deni au kumfidia mwajiri kwa hasara au uharibifu uliosababishwa na mfanyakazi. Kiwango cha jumla cha kipunguzo lazima kisiwe zaidi ya robo nusu ya ujira wa mfanyakazi.

Mwajiri anastahili kutoa risiti za malipo kwa wafanyakazi wote pamoja na malipo ya pesa taslimu au cheki; au kumpa mfanyakazi katika bahasha iliyofungwa iwapo ni pesa taslimu.

Vyanzo: Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004

Regulations on Work and Wages

  • Part V of Labour Institutions Act, No.7 of 2004 (through Regulation of Wages and terms of Employment Order, 2013 aka The Wage Order) / Sehemu ya tano ya Sheria ya Kanuni za Ajira na Mahusiano kazini namba 7 ya 2004 (kupitia Taratibu zamishahara na kanuni za Ajira (The Wage Order))
  • Employment and Labour Relations Act, No. 6 of 2004 / Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Sehemu ya 6 ya 2004

Loading...