Kima Cha Chini Cha Mishahara Zanzibari - Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je kuna sheria tofauti inayohusiana na kima cha chini cha mishahara Zanzibari?

Hakuna sheria tofauti inayohusiana na kima cha chini cha mishahara Zanzibari. kima cha chini cha mishahara huamuliwa na Bodi ya kima cha chini cha mishahara, iliyotolewa chini ya Sehemu 91 ya Sheria ya Ajira nambari 11 ya 2005.

Je kuna moja au zaidi ya kima cha chini cha mishahara kiliopo ambacho huamuliwa na sheria?

Kuna vima vya chini vya mishara viwili Zanzibari. Moja ya kitengo cha kibinafsi na ingine ya kitengo cha umma.

Ikiwa ndio, je vima hivi vya chini vya mishahara huamuliwa?

Vima vya chini vya mishara huamuliwa katika kiwango cha kitengo hiyo ni, kitengo cha kibinafsi na kitengo cha umma. Katika kitengo cha kibinafsi pia huamuliwa kulingana na kiwango cha ustadi.

Je kima cha chini cha mishahara huhesabiwa kivipi?

Chini ya sehemu 44 ya sheria ya ajira, Malipo ya kila siku (ya kudumu) hulingana na ustadi wa mfanyakazi. Kwa aliye na ustadi ni 10,000 Tsh na asiye na ustadi ni 7,000 Tsh kila siku (saa 42). Kwa wafanyakazi wa mkataba chini ya sehemu 44 ya sheria, mapato huamuliwa na Bodi ya kima cha chini cha mishahara chini ya Sheria ya Ajira Nambari. 3 ya sehemu ya 2005.

Katika hali ya kima cha chini cha mishahara cha kila wiki/kila mwezi, je hulingana na idadi ya saa zilizowekwa?

Saa za kazi ni saa 42 kila wiki - siku 6 za kazi katika wiki na saa 7 za kazi kila siku. Hata hivyo saa zinaweza kuongezewa hadi 45 baada ya makubaliano. Katika wajibu wa zamu muda unaweza kuongezwa hadi saa 48 kila wiki.

Je, mashirika ya serikali, mwajiri na/au washirika wa chama cha wafanyakazi wanahusika katika mpango wa kuweka kima cha chini cha mishahara?

Mashirika ya serikali, Wizara ya Kazi, Mashirija ya mwajiri, kama ZANEMA na mashirika ya Vyama vya wafanyakazi/chama cha mfanyakazi, kama ZATUC zinahusika katika kuweka Vima vya chini vya mishara. Wizara ya Fedha, Chama cha Wafanya biashara, Idara ya Huduma ya Umma, wataalamu 3 waliochaguliwa na Wizara ya Kazi pia wanahusika katika kuweka mapato.

Je ustawishaji (Marekebisho) wa kima cha chini cha mishahara huamuliwa aje?

Ustawishaji katika Vima vya chini vya mishara inaamuliwa kwa pamoja na serikali, mwajiri na wawakilishi wa chama cha wafanyakazi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi.

Taja sehemu za kima cha chini cha mishahara Zanzibari?

Kuna sehemu za kudumu tu za vima vya chini vya mishara.

Je, kijenzi cha kudumu cha kima cha chini cha mishahara hupandishwa daraja mara ngapi?

Kijenzi cha kudumu cha vima vya chini vya mishara hupandishwa daraja kila mwaka kama ilivyotajwa katika Sehemu IX ya Sheria, Bodi ya kima cha chini cha mishahara hukutana mara moja kwa mwaka. Mchakato wa kupandisha daraja ni ufatavyo. 94.(1) Bodi ya Ushauri wa Mapato itashauri Waziri kuhusu mapato na masuala mengine yanayohusiana na malipo ya mapato na upunguzaji mapato katika kitengo cha umma na cha kibinafsi kuhusu (a) mapato; (b) mapendekezo ya kutatua Vima vya chini vya mishara; (4) Bodi ya Ushauri wa Mapato ikitekeleza wajibu wake itaangalia sababu zifuatazo, kati ya zingine - (a) uwezo wa kulipa mapato; (b) gharama ya maisha: athari kwenye ajira, upunguzaji umaskini na utendaji wa biashara ndogo. 95.(1) Bodi ya Ushauri wa Mapato itakutana angalau mara moja kila mwaka.

Ni kipimo kipi ambacho ustawishaji kima cha chini cha mishahara hufanywa?

Viwango vya kuishi vyema huchukuliwa kama kipimo wakati wa kurekebisha viwango vya kima cha chini cha mishahara.

Kiwango cha Umasikini Kitaifa ni kipi? (katika sarufi ya kitaifa)

Kiwango cha umasikini wa kitaifa ni Tsh 1600

Kiwango cha Umasikini hupandishwa daraja mara ngapi?

Kiwango cha umasikini hupandishwa daraja kila mwaka.

Kiwango cha umasikini kilipandishwa daraja mara ya mwisho lini? (Bainisha MMMM/MM)

Kiwango cha umasikini hupandishwa daraja kila mwaka.

Ufikiano wa kima cha chini cha mishahara hudhibitiwa aje?

Ufikiano wa kima cha chini cha mishahara huthibitiwa na Wizara ya Kazi.

Ni vikwazo vipi vya kisheria vinaweza kutumika ikiwa hakuna maafikiano?

Sheria ya Ajira nambari 11 ya 2005 inaweza kutumika katika uafikiano. 22.(1) Kamishna, mkaguzi wa ofisi ya kazi au Kazi aliye na idhini ya Mwendesha mashtaka atakuwa na uwezo wa kuanzisha utaratibu wa jinai mbele ya mahakama yeyote katika kushindiwa kutii na miongozo ya sheria iliyotolewa chini au uvunjaji wa sehemu yeyote ya Sheria hii au sheria zingine zozote za kazi. Kulingana na 106(4) Mwajiri anayelipa mapato chini ya viwango vilivyoagizwa na Waziri, atakuwa na hatia ya kosa na baada ya kuhukumiwa atalipa faini isiyo chini ya shilingi elfu mia nne au kifungo kisicho chini ya miezi mitatu.

Je vikwazo hutumika mara kwa mara?

Vikwazo havitumiki mara kwa mara.

Je waakilishi wa mwajiri na au chama cha wafanyakazi huhusika katika utaratibu wa kuafikiana?

Ndio vyama vya wafanyakazi na waakilishi wa mwajiri wanahusika katika utaratibu wa kuafikiana.

Ni kwa nani/wapi watu binafsi wanaweza kulalamika, ikiwa wanafikiria wanapokea mapato ya chini kuliko kima cha chini cha mishahara?

Mtu binafsi anaweza kulalamika kwa Wizara ya Kazi na Huduma za Umma ikiwa anafikiria anapokea chini ya kima cha chini cha mishahara.

Ni mwezi upi wa mwaka kiwango cha kima cha chini cha mishahara hurekebishwa katika nchi yako?

kima cha chini cha mishahara hurekebishwa Desemba kila mwaka.


Loading...